What's Hot

    Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Patrice Motsepe amesema CAF haina mpango wa kuhamisha Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2027), hivyo zitabaki kwa nchi za Tanzania, Kenya na Uganda kama zilivyopangwa hapo awali.

    Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, baada ya kufanya ukaguzi wa maendeleo ya maandalizi ya fainali za AFCON katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Motsepe alisema pamoja na kuwepo minong’ono kuhusu kudorora kwa maandalizi hayo, amewatoa wasiwasi Watanzania kuwa hawana mpango wa kuhamisha fainali hizo.

    Motsepe amesema CAF hawana mpango B wala C, tofauti na waandaaji wa sasa Tanzania, Kenya na Uganda, hivyo fainali hizo hazitakuwa na mabadiliko yoyote.

    Alisema maandalizi yanaenda vizuri na kwenye kasoro ndogondogo zitarekebishwa na fainali hizo zitafanyika, huku akiahidi kurudi tena nchini Januari mwakani kwa ajili ya ukaguzi wa mwisho.

    Share.