Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Walace Karia amefungua kozi ya waamuzi ya Football Video Support (FVS) huku akiahidi mafunzo hayo kufanyika mara kwa mara.

    Akizungumza wakati ya ufunguzi wa kozi hiyo ya siku mbili inayofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Karia alisema ujio wa mfumo huo umekuwa msaada mkubwa kwa waamuzi na wadau wa mpira wa miguu kwa ujumla.

    Karia alisema kabla ya kuanza kutumika kwa mfumo huo mpira ulikuwa na lawama nyingi, lakini kwa sasa FVS imeondoa misuguano iliyokuwa hapo awali.

    Pia amewataka waamuzi kuwasikiliza makocha wanapoomba tukio fulani kurudiwa, watekeleze maombi hayo na kuacha FVS iamue itoe maamuzi sahihi juu ya tukio husika.

    Alisema baada ya kumaliza mafunzo hayo FVS itaanza kutumika rasmi chini ya waamuzi wa Tanzania, huku akiwaomba wafanye maamuzi kwa haraka pindi watakapoombwa kurudia tukio.

    Share.