Clara Luvanga afunguka baada ya kutua Washington Spirit
Mshambuliaji wa Tanzania, Clara Luvanga amefunguka ya moyoni baada ya kufanikiwa kutua katika Ligi ya Taifa ya Soka ya Marekani (NWSL) akijiunga na Washington Spirit kwa mkataba wa miaka minne.
Luvanga ambaye ni nyota wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania (Twiga Stars), amesema ana furaha kujiunga na timu hiyo, akijua kuwa anakwenda kukutana na changamoto mpya katika timu kubwa na yenye mafanikio.
Muda mchache baada ya kutambulishwa alisema: “Nina furaha sana kujiunga na Washington Spirit na kukabiliana na changamoto hii mpya katika NWSL.
“Najua nimewasili wakati msimu tayari unaendelea, lakini nina furaha kucheza katika ligi hii na nchi mpya. Timu iko katika nafasi nzuri na nataka kusaidia kwa kila namna niwezavyo hadi kufikia hatua ya mchujo.


