Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Miguel Gamondi amefurahishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake kwenye mechi dhidi ya Nigeria.
Gamondi ametoa kauli hiyo baada ya mechi ya kufuzu Pamoja AFCON 2027 iliyochezwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar na kumalizika kwa suluhu 0-0.
Taifa Stars mpaka sasa imeshacheza mechi nne ikikusanya pointi mbili huku ikibaki na mechi mbili.
Mechi mbili zilizobaki za Taifa Stars za Kundi L ni dhidi ya Guinea Bissau itakayochezwa Machi 24, 2027 ugenini na dhidi ya Madagascar Machi 28, 2027 nyumbani.


