Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL), Simba Queens wamebanwa na Ceasiaa Queens baada ya kutoka suluhu 0-0 katika mechi ya raundi ya nne iliyochezwa kwenye Uwanja wa KMC jijini Dar es Salaam.
Katika mechi nyingine, JKT Queens iliitandika Fauntain Gate Princess kwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Mej. Gen. Isamuyo jijini Dar es Salaam.
Mabao ya JKT Queens yalifungwa na Donisia Minja dakika ya 19, Bahati Kisanguzi dakika ya 73 na Alia Salum dakika ya 90.
Bunda Queens wakiwa nyumbani Uwanja wa Karume, Musoma wameibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Geita Queens.


