Futsal yapangwa kundi B AFCON
Timu ya Taifa ya wanaume ya Futsal imepangwa kundi B katika Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) zitakazofanyika nchini Morocco.
Tanzania imepangwa kundi B katika michuano hiyo itakayoanza tarehe 12 hadi 21 Oktoba mwaka huu ikijumuisha nchi nane kutoka kanda zote za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Timu nyingine za kundi B ni Misri, Angola pamoja na Msumbiji.
Kundi A linaundwa na timu ya Morocco ambaye ndiye bingwa mtetezi wa michuano hiyo akishinda taji hilo mara tatu (mwaka 2006, 2016 na 2024).
Timu ya Algeria, Zambia na Libya nazo zinaungana na Morocco katika kundi A.
Tanzania ilifuzu kushiriki fainali za Futsal AFCON 2026 baada ya kuifunga timu ya Ivory Coast katika mechi ya mwisho ya kufuzu kwa jumla ya mabao 9-7 chini ya uongozi wa Kocha Curtis Reid.


