What's Hot

    Yanga yatwaa Ngao ya Jamii 2026

    Young Africans (Yanga) ndiyo washindi wa Ngao ya Jamii kwa mwaka 2026.

    Timu hiyo iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi hiyo ya kuzindua mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa msimu wa 2025/2026.

    Bao pekee la dakika ya 32 kupitia kwa Mzambia Albert Kangwanda lilitosha kuipa Yanga ushindi katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa New Amaan, Zanzibar, Agosti 12 kuanzia saa 2.30 usiku.

    Mechi hiyo ya Ngao ya Jamii iliwakutanisha mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC (Yanga), na mabingwa wa Kombe la Shirikisho la CRDB (Simba).

    Share.