Karia awataka makatibu kusimamia maendele
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), amewataka makatibu wa vyama vya mikoa kutekeleza mipango ya maendeleo ya mchezo huo katika maeneo yao.
Akifungua kikao kazi kati ya TFF na makatibu hao tarehe 22 Agosti 2026 jijini Tanga, Rais alisema bila kusimamia majukumu yao kikamilifu hakutakuwa na muunganiko wa utekelezaji kati ya mikoa na TFF.
Kikao hicho kilichofanyika katika Kituo cha Ufundi cha TFF kilihudhuriwa na makatibu kutoka mikoa 23.
Wawezeshaji katika kikao hicho walikuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Oscar Mirambo, Mkurugenzi wa Sheria, Habari na Masoko wa TFF, Boniface Wambura, na Mkurugenzi wa Fedha wa TFF, Hassan Njama.
Mada zilizowasilishwa ni Utawala katika mpira wa miguu, maendeleo ya mpira wa miguu, na kanuni za fedha.


