Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania U23, Ahmad Ally amesema anaamini kwenye kufanikiwa katika mchezo wa kesho wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika AFCON 2027 dhidi ya Kenya, utakaochezwa Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

    Ahmad ametoa kauli hiyo leo alipokuwa anazungumza kwenye mkutano wa wanahabari uliofanyika Makao makuu ya TFF leo Oktoba 5, 2026.

    Kocha huyo alisema wamehamishia akili na nguvu zote kwenye mchezo wa marudiano kuhakikisha kazi iliyombele yao inatimia kwa kufanikiwa kufuzu kwenye hatua inayofuata.

    “Naamini kwenye kufanikiwa hivyo matokeo ya machezo wa kwanza tumechukua kama changamoto ya kuongeza morali ya kupambana,” alisema kocha huyo.

    Itakumbukwa timu ya Tanzania inahitaji ushindi pekee kwenye mchezo huo kwa magoli yasiyopungua matatu baada ya kupoteza kwa magoli 4-1 kwenye mchezo wa kwanza ugenini.

    Endapo Tanzania itafanikiwa kusonga mbele itakutana na Ivory Coast kwenye hatua inayofuata.

    Share.