Timu ya Taifa ya Tanzania U17 (Serengeti Boys) inaelekeza nguvu katika mchezo wale wa mwisho dhidi ya Mexico katika michuano ya Kombe la Vertex baada ya kupoteza kwa Argentina kwa mabao 3-2.
Mabao ya Serengeti Boys yalifungwa na Soann Adam aliyefunga bao la kwanza wakati bao la pili likifungwa na Luqman Mbalasalu.
Serengeti Boys inahitaji ushindi katika mchezo wa mwisho dhidi ya Mexico utakaochezwa Oktoba 7, 2026 ili kujihakikishia kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.


