Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi Tanzania, Cornel Barnabas amesema Mfumbo wa Football Video Support (FVS) sasa utatumika katika michezo yote 240 ya Ligi Kuu ya NBC, baada ya kupata ruhusa ramsi kutoka kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA).

    Mkurugenzi huyo amesema baada ya kukamilisha taratibu zote walizotakiwa kufanya kwa mwongozo wa Fifa, wameruhusiwa rasmi kutumia FVS  huku wakitakiwa kutoa ripoti kwa shirikisho hilo jinsi inavyotumika ili iwe sehemu ya kujifunza kwa nchi nyingine.

    Alisema FVS itaanza kutumia Oktoba 8, 2026 ligi hiyo itakaporejea na michezo 150 kati ya 240 ndiyo itakayotolewa ripoti yake Fifa, huku mchezo wa Simba na Yanga ukiwa mmoja wapo utakaoripotiwa kwa shirikisho hilo.

    Barnabas alisema kila timu itakuwa na kadi mbili za kuomba mapitio ya tukio ndani ya sekunde 60 baada ya kutokea, huku utaratibu maalum ukitumika pale maombi yote mawili yanapotumika.

    Kuelekea mchezo wa Derby Simba na Yanga, Barnabas amewataka mashabiki kukata tiketi mapema ili kuepuka usumbufu wa dakika za mwisho na mfumo wa ukataji tiketi utafunguliwa kesho, huku Uwanja wa Uhuru ukiwa na viti vyenye namba.

    Share.