Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.
Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi katika kikao chake cha
Machi 7, 2019 ilipitia matukio mbalimbali ya Ligi pamoja na malalamiko yaliyowasilishwa mbele yake na kufanya uamuzi ufuatao;
Mechi namba 244- Kagera Sugar 0 vs Mbeya City 1.
Kocha wa Mbeya City, Ramadhan
Nsanzurwimo amepewa Onyo Kali kwa kutoa maelekezo kwa timu yake wakati akiwa
jukwaani akitumikia adhabu ya kufungiwa katika mechi hiyo iliyofanyika Februari 6,
2019 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Adhabu dhidi yake imetolewa kwa
kuzingatia Kanuni ya 41(13) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha.
Mechi namba 245- Azam FC 1 vs Alliance FC 1. Kocha Malale Hamsini wa Alliance FC
amefungiwa mechi mbili na kutozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya
kuondolewa kwenye benchi la ufundi kwa kosa la kwenda kwenye uzio unaotenganisha
wachezaji na washabiki, na kuanza kuzozana na washabiki wa Azam FC katika mechi
hiyo iliyofanyika Februari 6, 2019.
Adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 41(11) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha.
Mechi namba 251- JKT Tanzania 0 vs Yanga 1. Klabu ya Yanga imetozwa faini ya sh.
1,500,000 (milioni moja na nusu) kutokana na timu yake kutoingia vyumbani wakati
wa ukaguzi na wakati wa mapumziko katika mechi hiyo iliyochezwa Februari 10, 2019
kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya
14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mechi namba 265- Mbeya City 1 vs Stand United 1.
Mchezaji Yusuph Abdallah wa
Mbeya City amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa
kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Stand United katika mchezo huo uliofanyika
Februari 15, 2019 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya.
Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 38(9) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.
Mechi namba 270- Yanga 0 vs Simba 1.
Klabu ya Yanga imetozwa faini ya jumla ya
sh. 6,000,000 (milioni sita) kwa kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi,
kutoingia vyumbani na kusababisha wachezaji wakaguliwe kwenye korido, na pia
kutotumia njia maalum iliyowekwa kwa ajili ya kuingia kwenye eneo la kuchezea
(pitch) katika mechi hiyo iliyochezwa Februari 16, 2019 katika Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Nayo Simba imetozwa faini ya sh. 3,000,000 (milioni tatu) kwa kuingia uwanjani
wakitumia mlango usio rasmi, lakini vilevile kutotumia njia maalum iliyowekwa kwa
ajili ya kuingia kwenye eneo la kuchezea (pitch).
Adhabu kwa timu zote zimetolewa
kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mechi namba 272- Mwadui FC 2 vs Biashara United 1.
Klabu ya Biashara United
imetozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kuvamia
chumba cha timu ya Mwadui FC kutokana na imani za kishirikina katika mechi hiyo
iliyochezwa Februari 19, 2019 kwenye Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.
Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 43(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu.
Mechi namba 274- Mbao FC 1 vs Yanga 2. Klabu ya Yanga imetozwa faini ya sh.
500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kuvamia eneo la kuchezea (pitch)
kushangilia ushindi mara baada ya kumalizika mechi hiyo iliyofanyika Februari 20,
2019 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Adhabu hiyo imezingatia Kanuni
ya 43(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu.
Mechi namba 275- Ndanda 2 vs Singida United 0.
Kocha Dragan Popadic wa Singida
United FC amefungiwa mechi mbili na kutozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada
ya kuondolewa kwenye benchi la ufundi kwa kosa la kupinga maamuzi ya Mwamuzi
katika mechi hiyo iliyofanyika Februari 20, 2019 kwenye Uwanja wa Nangwanda
Sijaona, Mtwara.
Adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 41(11) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha.
Mechi namba 277- Coastal Union 1 vs Azam FC 1.
Kocha wa Azam FC, Hans van
Pluijm na wachezaji wake Ramadhan Singano, na Stephen Kingue wamepelekwa
Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kuwavamia na kuwazonga waamuzi katika eneo la
kuchezea (pitch) baada ya filimbi ya mwisho katika mchezo huo uliofanyika Februari
19, 2019 kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Mechi namba 162- Azam FC 1 vs Simba 3. Klabu ya Azam imetozwa faini ya sh.
3,000,000 (milioni tatu) kwa kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi, na
kutoingia vyumbani hivyo kusababisha wachezaji wakaguliwe kwenye korido katika
mechi hiyo iliyochezwa Februari 22, 2019 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi namba 283- Ruvu Shooting 6 vs Mwadui FC 2.
Kocha Ally Bizimungu wa
Mwadui FC amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada
ya kuwazonga waamuzi vyumbani mwao kabla ya kuanza kipindi cha pili, na pia
kumfokea Mwamuzi Msaidizi, hivyo Mwamuzi kumtoa kwenye benchi katika mechi hiyo
iliyofanyika Machi 2, 2019 kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi, Pwani.
Adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 41(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha.
Mechi namba 288- Kagera Sugar 2 vs Lipuli 0. Kocha Msaidizi wa Lipuli FC, Selemani
Matola amefungiwa mechi mbili na kutozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya
kuondolewa kwenye benchi la ufundi kwa kosa la kupinga maamuzi ya Mwamuzi katika
mechi hiyo iliyofanyika Machi 3, 2019 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 41(11) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha Ligi.
Daraja la Kwanza.
Mechi namba 80- Mawenzi SC 1 vs Mlale FC 1.
Klabu ya Mlale FC imetozwa faini ya
sh. 500,000 (laki tano) baada ya washabiki wake kuwavamia wale wa Mawenzi SC na
kuanza kuwapiga katika mechezo huo uliofanyika Februari 16, 2019 kwenye Uwanja
wa Jamhuri mjini Morogoro.
Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 43(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti kwa Klabu.
Naye Kamishna wa mechi hiyo, Bw. Nassoro Kipenzi kutoka Dodoma ameondolewa
kutokana na ripoti yake kuwa na upungufu kuhusu tukio hilo.
Mechi namba 84- Mbeya Kwanza 1 vs Reha FC 0.
Mchezaji Idrissa Ramadhan Ally wa
Reha FC amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kosa la kumpiga kichwa
mchezaji mmoja wa Mbeya Kwanza katika mechi hiyo iliyofanyika Februari 16, 2019
kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Nayo klabu ya Mbeya Kwanza imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya
washabiki wake kuvamia uwanja (pitch) kushangilia bao la timu hiyo.
Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 43(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti kwa Klabu.
Mechi namba 73- Pamba SC 1 vs Transit Camp 0.
Klabu ya Transit Camp imetozwa
faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na viongozi wa benchi la ufundi kumzonga
Mwamuzi baada ya mchezo huo uliofanyika Februari 9, 2019 kwenye Uwanja wa
Nyamagana jijini Mwanza.
Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 43(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti kwa Klabu.
Mechi namba 74- Polisi Tanzania 1 vs Geita Gold 0.
Klabu ya Polisi Tanzania
imetozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kufanya vitendo vilivyoashiria imani za
kishirikina ikiwemo kuvunja mayai kwenye kona ya uwanja katika mchezo huo
uliofanyika Februari 9, 2019 kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.
Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 43(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti kwa Klabu.
Mechi namba 76- Rhino Rangers 0 vs Dodoma FC 0.
Klabu ya Dodoma FC imepewa
Onyo baada ya kuchelewa kuingia uwanjani kwa dakika 16 katika mchezo huo
uliofanyika Februari 9, 2019 Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mechi namba 80- Arusha United 1 vs Green Warriors 0.
Klabu ya Green Warriors
imetozwa faini ya sh. 1,500,000 (milioni moja na nusu) kwa timu yake kugoma kuingia
vyumbani, hivyo kusababisha ikaguliwe ikiwa nje katika mchezo huo uliofanyika
Februari 16, 2019 Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.
Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za
Mchezo.
Mechi namba 82- Mgambo Shooting 0 vs Pamba SC 1.
Mchezaji Rashid Ally wa
Mgambo Shooting amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kosa la kumpiga kiwiko
mchezaji Elias Seth wa Pamba SC baada ya kumalizika mchezo huo uliofanyika
Februari 16, 2019 Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Mechi namba 88- Mashujaa FC 2 vs Pamba SC 1.
Mchezaji Deus Tulusubya wa Pamba
SC amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kosa la kutaka kuwapiga waamuzi
katika nyakati tofauti kwenye mchezo huo uliofanyika Machi 2, 2019 Uwanja wa Lake
Tanganyika mjini Kigoma.
Ligi Daraja la Pili
Mechi namba 29- Ihefu FC 2 vs Kitayosce FC 1.
Kocha Isack Gamba wa Kitayosce FC,
amefungiwa mechi mbili na kutozwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) baada ya
kuondolewa kwenye benchi la ufundi kwa kosa la kutoa lugha chafu kwa waamuzi
katika mechi hiyo iliyofanyika Januari 12, 2019 Uwanja wa Highland Estate, Mbeya.
Adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 41(11) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Udhibiti
kwa Makocha.
Mechi namba 32- Usalama FC 1 vs The Might Elephant FC 1.
Daktari wa The Might
Elephant, Bw. Shaban Sengo amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kosa la
kuingilia ugomvi kati ya washabiki wa timu yake dhidi ya wale wa Usalama FC kwenye
mchezo huo uliofanyika Januari 12, 2019 kwenye Uwanja wa Singe Sekondari mjini
Babati.
Mechi namba 29- Kasulu Red Star FC 0 vs Area C United 0.
Kipa wa akiba wa Area C
United, Abdul Mohamed amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kosa la kumpiga
Kamishna na kutoa lugha ya matusi katika mchezo huo uliofanyika Januari 12, 2019
Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Mechi namba 37- Kumuyange FC 2 vs Kasulu Red Star FC 2.
Mchezaji wa Kasulu Red
Star, Timotheo T. Gugamwa amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kosa la
kujaribu kumpiga Mwamuzi katika mchezo huo uliofanyika Februari 2, 2019 Uwanja wa
Kabanga Sekondari ulioko Ngara, Kagera.
Mechi namba 45- Toto Africans 2 vs Milambo FC 1.
Klabu ya Milambo FC imepewa
Karipio Kali baada ya kuchelewa kufika uwanjani kwa nusu saa katika mchezo huo
uliofanyika Februari 17, 2019 Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 14(48) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mechi namba 48- Area C United 0 vs Kumuyange FC 0.
Klabu ya Kumuyange FC
imetozwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kutokana na timu yake kutohudhuria kikao
cha maandalizi ya mechi (pre match meeting) kwa ajili ya mchezo huo uliofanyika
Februari 17, 2019 Uwanja wa Kibaigwa, Dodoma.
Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya
14(3) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Taratibu za Mchezo.
Naye Meneja wa Kumuyange FC, Joseph Sinzo amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF
baada ya kumwaga maji kwenye chumba cha kubadilishia cha timu ya Area C United.
Mechi namba 32- African Sports 1 vs Changanyikeni Rangers FC 0.
Kamishna Beda Lyimo na Mwamuzi Sebastian Sanga wamepewa Onyo kutokana na ripoti zao kuwa na upungufu katika mchezo huo uliofanyika Januari 15, 2019 Uwanja wa Nyamagana
jijiniMwanza.
Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 14(48) ya Ligi Daraja la Pili.
Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.