Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

LIGI Kuu ya Wanawake ya Serengeti Premium Lite inatarajia kuanza Jumamosi , Disemba 29,2018 ikishirikisha timu 12.

Ligi hiyo itachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.

Akizungumza kuelekea kwenye uzinduzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Serengeti Premium Lite,Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Wanawake Amina Karuma amesema msimu huu utakua na ushindani mkubwa.

Amesema kwa namna timu zote zilivyojiandaa na kwa udhamini wa kinywaji cha Serengeti Lite,inaifanya ligi kuongeza ushindani zaidi.

“Ni ukweli usiopingika kwamba ligi yetu ya wanawake ambayo inadhaminiwa na Serengeti Premium Lite inaongezeka chachu ya ushindani na tunatarajia msimu unaoanza utakua na ushindani zaidi” amesema Karuma.

kwa upande wake, Afisa masoko wa Serengeti Breweries Bw. George Mango amesema wamejiandaa vya kutosha kuwezesha mashindano hayo kuonesha msisimko ili kuwapatia burudani mashabiki wa mpira wa miguu pamoja na kutoa ushindani mkubwa wa soka la wanawake kupitia bia murua ya Serengeti Premium Lite.

“Serengeti Breweries Limited kupitia kinywaji chake cha Serengeti Premium Lite imewekeza kiasi cha Shilingi milioni 450 ili kuwezesha ligi hii ya wanawake iwe ya ushindani mkubwa na kuwaletea msisimko mashabiki wa soka hapa nchini,” alisema George na kubainisha kwamba maandalizi ya kuwezesha michuano hiyo yamekamilika.

“Watanzania wakae tayari sasa kuona burudani maridhawa kutoka kwa timu zinazoshiriki ligi hii. Hakika ni ligi inayotarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu sana,” alisema. “Tumeona namna ambavyo ligi ilivyoweza kutoa misisimko na msimu huu timu zimeongezeka kutoka 8 kwenye ligi mwaka jana hadi 12 za sasa,”

Bia ya Serengeti Lite ni kinywaji murua kinachozalishwa na kampuni ya Serengeti Breweries Limited. Mbali na bia hii, Serengeti Breweries pia hutengeneza na kusambaza vinywaji mbalimbali, ikiwemo bia ya Serengeti Premium Lager, iliyojizoelea tuzo kadhaa za kimataifa kwa ubora, inayodhamini timu ya taifa ya mpira wa miguu, Taifa Stars.

Timu 12 zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite Tanzania Bara ni:

1. KIGOMA SISTERZ- KIGOMA
2. SIMBA QUEENS – DSM
3. ALLIANCE GIRLS –MWANZA
4. BAOBAB QUEENS – DODOMA
5. MLANDIZI QUEENS – PWANI
6. JKT QUEENS – DSM
7. PANAMA – IRINGA
8. EVERGREEN –DSM
9. MARSH ACADEMY – MWANZA
10. MAPINDUZI QUEENS – NJOMBE
11. YANGA PRINCESS –DSM
12. TANZANITE – ARUSHA.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.