Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Waziri Ndumbaro Amesisitiza Hamasa Timu za Taifa

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mh. Damas Ndumbaro ametoa rai kwa watanzania wote kuunganan na Serikali pamoja na TFF katika kuzisapoti timu za Taifa hasa zile zilizo fuzu kushiriki michuano ya Afrika (AFCON na WAFCON).

Aliyasema hayo wakati wa mkutano mkuu wa 10 wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania ambao umefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa NSSF Mafao House jijini Dar es Salaam Disemba 8, 2023.

Akifungua mkutano huo wa 10 mgeni rasmi, Mh Ndumbaro aliwataka wtanzania kwa ujumla kujitoa ka namna wanayo weza katika kuzisapoti timu hizo ambapo pia amemuagiza katibu mkuu Baraza la Michezo BMT Neema Msitha kutengeneza miundombinu rahisi ya watanzania walio tayari kuzisapoti timu hizo.

“ Tunatambua kwamba timu zetu mbili zinazokwenda kushiriki AFCON na WAFCON ni mzigo mkubwa TFF peke yao hawawezi hivyo wadau wanahitajika tar 2/5 hapa jijini Dar es Salaam kutafanyika fund raising tunataka michango yenu,” alisema

 

Aidha amewataka wachezaji ambao walishiriki AFCON ya kwanza mwaka 1980 wawepo kwani wao ndio waanzilishi wa njia hiyo na kwamba bado ushauri wao unahitajika, pia alisema siku hiyo zitanadiwa jezi za hao wachezaji wawe hai ama wameshatangulia mbele za haki.

 

Aidha alisema itaundwa kamati ya hamasa kwa timu zote mbili Twiga Stars na Taifa Stars ambapo umetolewa mwanya kwa watanzania kutuma maombi kwenye baraza la michezo (BMT ) kwa mtanzania anayeona anaweza kuhamasisha kwani jambo la kila mmoja.

Viongozi wengine waliohudhulia mkutano huo ni Makamu wa Kwanza wa Rais TFF Athumani Nyamlani, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Steven Mnguto, Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania Neema Msitha, Katibu Mkuu wa TFF Kidao Wilfred,  na viongozi wengine kutoka TFF, Bodi ya Ligi na wawakilishi wa timu zinazo shiriki Ligi kuu ya NBC, Championship na First Division League.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.