Mchezo wa kirafiki kwenye kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kati ya Morocco na Tanzania (Taifa Stars) uliopangwa kuchezwa Oktoba 5, 2026 nchini Morocco umefutwa.

    Uamuzi wa kufuta mchezo huo umetokana na ripoti ya madaktari wa Taifa Stars wakati wakielezea hali ya wachezaji waliopo kambini kwenye mji wa Tangier, niching Morocco.

    Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wachezaji watano (5) wamepata majeraha ambayo yatawafanya washindwe kucheza mchezo huo dhidi ya Morocco, hivyo baada ya kushauriana na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Miguel Gamondi wakakubaliana kuufuta mchezo huo.

    Taifa Stars ilisafiri na wachezaji 23 pekee kwa mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 dhidi ya Madagascar uliochezwa Meknès, Morocco Septemba 29, 2026 na baada ya mchezo huo walitakiwa kucheza mchezo huo wa kalenda ya FIFA.

    Tayari wachezaji na benchi la Ufundi wamepewa taarifa ya kufutwa mchezo huo.

    Share.