Fainali ya Ngao ya Jamii itazikutanisha timu ya Simba Queens na JKT Queens baada ya timu hizo kushinda kwenye michezo yao ya Nusu Fainali Septemba 30, 2026, iliyochezwa kwenye Uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam.
JKT Queens ilishinda goli 1-0 dhidi ya Mashujaa Queens kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza kabla Simba Queens kushinda magoli 3-0 dhidi ya Yanga Princess kwenye nusu fainali ya pili.

Hata hivyo timu zote hizo nne zinakwenda kujipanga kwa ajili ya michezo ya mwisho itakayochezwa Oktoba 3, 2026 hapo hapo KMC Complex.
Kukamilisha fainali hizo Itachezwa michezo miwili ambapo Mashujaa Queens atamenyana na Yanga Princess kupata mshindi wa tatu, huku mchezo wa fainali ukizikutanisha timu za Simba Queens na JKT Queens kupata bingwa wa Ngao ya Jamii 2026.


