Timu ya Taifa ya Tanzania U17 (Serengeti Boys) leo inashuka uwanjani kuvaana na China katika mchezo wa kwanza wa michuano ya Kombe la Vertex inayofanyika jijini London nchini Uingereza.

    Serengeti Boys inatumia mashindano hayo yanayoanza leo Oktoba 1, 2026 na kumalizika Oktoba 7 mwaka huu kama sehemu ya maandalizi ya Kombe la Dunia litakalofanyika nchini Qatar mwezi Novemba 2026.

    Katika michuano hiyo, Serengeti Boys itacheza michezo mitatu, ambapo baada ya mechi ya leo dhidi ya China, itakutana na Argentina mchezo utakaochezwa Oktoba 4, 2026 na mchezo wa mwisho itamalizana na Mexico Oktoba 7, 2026.

    Bingwa katika michuano hiyo atapatikana kwa kukusanya alama nyingi katika michezo mitatu, hivyo Serengeti Boys inatakiwa kukusanya alama zote katika michezo watakayocheza.

    Share.