Timu ya Taifa ya Wavulana U15 imemaliza michuano ya Kombe la Dunia iliyokuwa inafanyika Baku nchini Azerbaijan kwa mafanikio.
Katika michuano hiyo Tanzania ilicheza mechi 11 ambapo kati ya hizo walifanikiwa kuibuka na ushindi katika mechi sita, kupoteza nne huku ikitoka sare moja.
Kocha wa timu ya Tanzania, Mohamed Amin amesema michuano hiyo kwao imekuwa na faida kubwa, kwani pamoja na kutopata ubingwa lakini wamejifunza mambo mengi.
Amesema vijana wamepata uzoefu wa kucheza mechi kubwa kitu ambacho kitawajenga katika ukuaji wao wa kisoka, lakini hata benchi la ufundi wamejifunza mengi ambayo watayafanyia kazi siku za usoni


