Klabu ya Bunda Queens imeanza na rekodi ya kuwa timu ya kwanza kufunga bao msimu wa 2026/2027 wa Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) huku ikiwa timu ya kwanza kufunga mabao matano katika mchezo wa kwanza.
Bao la Jamila Selestine lililofungwa dakika ya 4 liliweka rekodi hiyo ya bao la kwanza kufungwa msimu huu katika mechi ambayo wameandika pia rekodi ya kupata ushindi mkubwa wa mabao 5-2, katika iliyochezwa kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Msimu wa Ligi ya TWPL umeanza rasmi leo Oktoba 28, 2026 kwa mechi sita kuchezwa na kuzikutamisha timu 12 katika viwanja sita tofauti.
Mechi nyingine zilizochezwa leo ni Mashujaa Queens iliyopata ushindi dhidi ya Fountain Gate Princess kwa mabao 3-1 katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma huku Mabingwa watetezi Simba Queens wakiitandika Kilimanjaro Wonders kwa mabao 3-0, kwenye Uwanja wa Ushirika, mjini Moshi.
Bunda Girls waliwakaribisha Yanga Princess katika Uwanja wa Karume mkoani Mara na kukukubali kichapo cha mabao 3-0, JKT Queens waliifunga Geita Queens kwa mabao 2-0, katika Uwanja wa Nyankumbu na Alliance Girls waliichapa Ceasiaa Queens kwa mabao 2-0.


