Timu ya Taifa ya Wavulana U15 imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Botswana katika mechi ya Kombe la Dunia zinazoendelea katika mji wa Baku nchini Azerbaijan.
Katika mechi hiyo mabao ya Tanzania yalifungwa na Seleman Msuya aliyefunga mawili, wakati Seleman Deus na Yasir Jumbe wakifunga bao moja kila mmoja.
Katika mechi ya awali iliyochezwa mapema leo, Tanzania ilipoteza kwa bao 3-1 dhidi ya Somalia, huku bao lao likifungwa na Shafii Kassimu.


