Timu ya Taifa ya Wavulana U17 (Serengeti Boys) imelazimisha sare ya 2-2 na Venezuela katika michuano ya U17 Dubai Youth Challenge.

    Katika mechi hiyo ya kwanza mabao ya Serengeti Boys yaliwekwa wavuni na Soann Adam na Faraji Kayanda.

    Mechi inayofuata ya Serengeti Boys itakuwa dhidi ya Australia Novemba 13, 2026, kabla ya kumaliza na Tajikistan Novemba 15, 2026.

    Serengeti Boys inashiriki michuano hiyo ikiwa sehemu ya maandalizi ya Kombe la Dunia 2026 kwa kucheza mechi tatu.

    Share.