Mchezaji wa JKT Queens ya Tanzania, Winfrida Gerald amechaguliwa kuwa miongoni mwa nyota 10 wa kike wanaowania Tuzo ya Mchezaji Chipukizi wa Soka la Wanawake kwenye Tuzo za CAF 2026.
Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika Desemba 7, 2026, jijini Lagos, Nigeria, ambapo mastaa waliofanya vizuri watakutana kupokea heshima zao katika vipengele vya mtu mmoja mmoja, timu za taifa pamoja na klabu.
Winfrida katika kinyang’anyiro hicho anakabiliwa na ushindani kutoka kwa nyota wengine wa kike barani Afrika ambao ni Romaine Gandonou (Benin), Maeva Nyadjou (Cameroon) na Grace-Ruth Sery na N’Sira Ouedraogo (Ivory Coast).
Wengine ni Rose Kadzere (Malawi), Kautar Azraf (Morocco), Seimeyeha Janet Akekoromowei na Oluwakemi Adegbuyi (Nigeria) na Adji Ndiaye (Senegal).


