Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL), Simba Queens wamejikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya kuichapa Mashujaa Queens kwa mabao 2-0, katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Mej. Gen. Mzee, jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba Queens katika mechi hiyo yalifungwa na Vivian Corazone aliyefunga dakika ya 43 na Zaina Nandede dakika ya 90+4, kuifanya timu yao kukusanya pointi 9.
Nafasi ya pili katika msimamo inashikiliwa na JKT Queens ikiwa na pointi 9, baada ya kuichapa Yanga Princess kwa bao 1-0, likifungwa na mshambuliaji wake Asha Rashid.
Katika mechi nyingine za raundi ya tatu, Bunda Girls iliichapa Geita Queens kwa mabao 2-0, Ceasiaa Queens wakiwa ugenini waliitandika Tausi FC kwa mabao 2-0.
Kilimanjaro Wonders walibanwa mbavu nyumbani na Fountain Gate Princess kwa kulazimishwa suluhu.


