Mechi tano za raundi ya tatu ya Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) 2026/2027 zinatarajiwa kuchezwa kesho Novemba 11, 2026 ambapo miamba 10 itashuka dimbani kusaka pointi tatu.
Bunda Girls watakuwa wenyeji wa Geita Queens katika Uwanja wa Karume mjini Mara, Tausi FC watawakaribisha Ceasiaa Queens mechi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Mechi nyingine za kesho, Kilimanjaro Wonders watakuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi kuwakabili Fountain Gate Princess wakati vinara wa ligi hiyo, Yanga Princess watavaana na JKT Queens mechi itakayopigwa Uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam.
Mabingwa watetezi Simba Queens watakuwa wageni katika Uwanja wa Meja Jenerali Mzee dhidi ya Mashujaa Queens, mechi zote zitapigwa saa 10 jioni.
Raundi hiyo ya tatu leo ilishuhudia mechi moja ikichezwa kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza ambapo Alliance Girls ikiwa nyumbani ililazimishwa sare ya mabao 2-2 na Bunda Queens.


