Timu ya Taifa ya Wavulana U17 (Serengeti Boys) imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tajikistan katika michuano ya U17 Dubai Youth Challenge.
Bao la Serengeti Boys Katika mechi hiyo limefungwa na Faraji Kayanda.
Ushindi huo ni wa kwanza kwa Serengeti Boys baada ya kutoka sare katika mechi mbili dhidi ya Venezuela mabao 2-2 na Australia 1-1.
Serengeti Boys imeshiriki michuano hiyo ikiwa sehemu ya maandalizi ya Kombe la Dunia 2026 litakalofanyika Qatar kuanzia Novemba 19, 2026.


