Wachezaji Benard Kamungo na Ben Starkie, wameongeza nguvu kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ( Taifa Stars) kinachojiandaa na mechi ya marudiano kufuzu PAMOJA AFCON 2027 dhidi ya Nigeria.

    Kamungo anayekipiga katika klabu ya FC Dallas ya Marekani na Starkie anayechezea timu ya Truro City ya England, wamejiunga kwenye kikosi na kushiriki mazoezi.

    Wachezaji hao wamejiunga na mwenzao kambini Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya mechi dhidi ya Nigeria itakayochezwa Novemba 17, 2026 kwenye Uwanja wa Amaan Complex, Zanzibar ya kufuzu PAMOJA AFCON 2027.

    Share.