Tanzania kuivaa Uganda fainali CECAFA U-17
Timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 17 (Serengeti Girls) imetinga hatua ya fainali ya mashindano ya CECAFA baada ya kuifunga Sudan Kusini mabao 4-0 katika nusu fainali iliyochezwa Juni 21 kwenye Uwanja wa KMC jijini Dar es Salaam.
Bahati Kizanguzi anayeongoza kwa ufungaji katika michuano hiyo alifunga mawili, na hivyo kufikisha mabao kumi.
Mabao mengine ya Serengeti Hirls yalifungwa na Harrier Juma, na Yasinta Kaluwa.
Kwa matokeo hayo Tanzania itacheza na Uganda katika fainali. Uganda imeingia hatua hiyo baada ya kuifunga Kenya mabao 3-0 katika mechi ya kwanza ya nusu fainali .
Baada ya mechi kumalizika Kocha wa Serengeti Girls, Esther Chabruma aliwapongeza wachezaji kwa kufika fainali, na kusema lengo la kutwaa ubingwa wa CECAFA lazima litimie.
Mashindano ya CECAFA yatamalizika Juni 23 ambapo fainali itachezwa saa 10:30 jioni huku mechi ya mshindi wa tatu kati ya Kenya na Sudan Kusini ikianza 7:00 mchana. Mechi zote zitachezwa Uwanja wa KMC.


