Timu ya Taifa ya Wanaume U20 (Ngorongoro Heroes) imeanza kwa kishindo michuano ya kuwania kufuzu Fainali za AFCON Kanda ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), kwa kuitandika Rwanda mabao 3-0, mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

    Mabao ya Ngorongoro Heroes yamefungwa na Faraji Kayanda dakika ya 30, kabla ya Djuma Abushiri kufunga bao la pili dakika ya 37, wakati msumali wa mwisho uligongelewa na Evastus Lukanima dakika ya 41.

    Ngorongoro Heroes watashuka tena uwanjani tarehe 19 Novemba 2026 watakapovaana na Ethiopita mchezo ambao wakishinda watakuwa wamekata tiketi ya kucheza nusu fainali ya michuano hiyo.

    Share.