Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni, Jarufu Juma amesema pamoja na kupata sare ya bao 1-1 katika mechi ya nyumbani, bado wana matumaini ya kufanya vizuri ugenini na kufuzu.
Jarufu amesema walipambana ili kupata ushindi kwa bahati mbaya wamepata sare, lakini watajipanga kufanyia kazi walichokiona kwenye mechi hiyo ili wakafanye vizuri ugenini.
Mechi ya marudiano unatarajiwa kuchezwa Oktoba 17, 2026 Maputo Msumbiji, ambapo wakifanikiwa kuibuka na ushindi watafuzu kucheza fainali za AFCON zitakazofanyika nchini Senegal.


