Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) imetamba ugenini baada ya kuichapa Botswana kwa bao 1-0 katika mchezo wa kuwania kufuzu Olimpiki Los Angeles 2028.

    Bao lililoipa Twiga Stars ushindi katika mchezo huo wa mkondo wa kwanza limefungwa na Oprah Clement dakika ya 60.

    Akizungumzia mchezo huo, Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Bakari Shime amesema mchezo ulikuwa mgumu lakini wachezaji wake walitekeleza majukumu yao na kuwapa ushindi.

    “Kipindi cha kwanza tulimaliza kwa sare, mapumziko nikawaambia wachezaji wangu wacheze kikubwa ili mchezo wa nyumbani usiwe na kazi kubwa, nashukuru wametekeleza,” alisema Shime.

    Twiga Stars inatarajiwa kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya Botswana Oktoba 13, 2026, jijini Dar es Salaam.

    Share.