Timu ya Taifa ya Tanzania U17 (Serengeti Boys) imeanza kwa kishindo michuano ya kuwania kufuzu AFCON 2027 Kanda ya CECAFA baada ya kuichapa Kenya kwa mabao 2-0.
Mabao ya Serengeti Boys yamefungwa na Dismass Athanas dakika ya 28 na bao la pili likifungwa na Godfrey Somi dakika ya 57.
Serengeti Boys ambayo ipo katika kundi C sambamba na Kenya na Somalia watashuka tena dimbani Oktoba 12 kuvaana na Somalia na wakifakiniwa kuibuka na ushindi watatinga hatua ya nusu fainali itakayochezwa Oktoba 17, 2026.
Timu zitakazotinga fainali zitakuwa zimekata tiketi ya kucheza fainali za AFCON 2027 zitakazofanyika nchini Morocco mwezi Aprili mwakani.


