Timu ya Taifa ya Wavulana U15 imezitandika Mauritius na Syria katika mechi mbili za Kombe la Dunia zilizochezwa leo Baku nchini Azerbaijan.
Katika mechi ya kwanza iliyocheza asubuhi Tanzania ilicheza na Mauritius na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.
Mabao ya Tanzania katika mechi hiyo dhidi ya Mauritius yalifungwa na Yasir Jumbe, Shafii Kassimu na Frank Hassan
Katika mechi ya pili iliyochezwa jioni, Tanzania iliwatandika Syria kwa mabao 5-2, mabao yakifungwa na Shafii Frank, huku Selemani Deus na Agustino lugobola wakifunga mabao mawili kila mmoja.


