Timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni imeondoka leo kuelekea Msumbiji kwa ajili ya mechi ya marudiano ya kufuzu AFCON 2026.
Tanzania inaifuata Msumbiji ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Oktoba 11, 2026, katika ufukwe wa JKT Mbweni (Ndege Beach) jijini Dar es Salaam.
Tanzania sasa inaelekeza nguvu zake katika mchezo huo muhimu, ikilenga kupata matokeo yatakayoipa nafasi ya kufuzu fainali za AFCON 2026 zitakazofanyika nchini Senegal kuanzia Novemba 7 hadi 15, 2026.


