Timu ya Taifa ya Tanzania ya Futsal kesho inatarajia kucheza mechi yake ya mwisho ya kundi B dhidi ya Msumbiji katika fainali za Futsal AFCON 2027 zinazochezwa kwenye uwanja wa CSPMA nchini Morocco.
Mechi hiyo ni muhimu kwa Tanzania ikiwa na lengo la kuvuna ushindi katika michuano hiyo, baada ya kupoteza katika mechi zake mbili zilizotangulia ikiwemo ya jana dhidi ya Angola ikipoteza kwa mabao 6-0.
Mashindano ya AFCON Futsal yanafanyika Rabat, Morocco yakishirikisha mataifa nane ya Tanzania, Misri, Angola na Msumbiji yaliyopo kundi B wakati kundi A lenyewe likiwa na Libya, Zambia, Algeria na wenyeji Morocco.


