Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wavulana U17 (Serengeti Boys) imeondolewa katika michuano ya kufuzu AFCON 2027 Kanda ya CECAFA kwa kurusha sarafu baada ya kufanana kila kitu na Somalia.
Serengeti Boys na Somalia zote zimefikisha pointi 4 baada ya wote kushinda kwa mabao 2-0 walipocheza na Kenya na mechi yao wenyewe walipokutana kumalizika kwa sare ya bao 1-1 na kufanya timu hizo kufanana kila kitu hivyo ili kupata timu moja ya kuingia nusu fainali ikalazimika kurushwa sarafu ambapo bahati ikaangukia kwa Somalia.
Kwa mujibu wa kanuni ya 13 kifungu c ya CAF inaeleza kuwa endapo timu zaidi ya mbili zitakuwa na usawa mwishoni mwa mechi za hatua ya makundi na kufungana kwa kila kitu, uamuzi utafanyika kwa kupiga kura ya bahati nasibu, utakaofanywa na Kamati ya Maandalizi.
Baada ya maamuzi hayo ya kuruşha sarafu, Somalia imefuzu hatua ya nusu fainali kwa kuongoza Kundi C, akiungana na Uganda iliyoongoza Kundi B na Rwanda walioongoza Kundi A wakati Ethiopia amefuzu kupitia mshindi wa pili mwenye matokeo mazuri (Best looser)


