Timu ya Taifa ya Tanzania ya Futsal inaelekeza nguvu zake katika mechi yake na Angola itakayochezwa kesho CSPMA, Morocco.

    Mechi hiyo ya Kundi B itakuwa ya pili kwa timu zote mbili baada ya mechi za kwanza zilizochezwa Oktoba 13 mwaka huu.

    Tanzania ilipoteza mchezo wa kwanza mbele ya Misri kwa mabao 8-0 wakati Angola wenyewe waliibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Msumbiji.

    Mashindano ya AFCON Futsal yanafanyika Rabat, Morocco yakishirikisha mataifa nane ya Tanzania, Misri, Angola na Msumbiji yaliyopo kundi B wakati kundi A lenyewe likiwa na Libya, Zambia, Algeria na wenyeji Morocco.

    Share.