Mwamuzi wa Tanzania Ahmed Arajiga ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kushiriki kozi ya waamuzi wa daraja la CAF Ellite A ikiwa ni maandalizi ya hatua ya makundi ya michuano ya CAF kwa ngazi ya klabu.

    Kozi hiyo ya siku sita inatarajiwa kufanyika jijini Cairo nchini Misri kuanzia Novemba 18 na kumalizika Novemba 23 2026.

    Arajiga ni miongoni mwa waamuzi 35 watakaoshiriki kozi hiyo ya kujiandaa na hatua ya makundi inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.

    Share.