Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua mwamuzi wa Tanzania, Ahmed Arajiga kuchezesha mechi ya kufuzu AFCON 2027 kati ya Equtorial Guinea na Zimbabwe, itakayochezwa katika Uwanja wa Yaounde Omnisports Ahm, nchini Cameroon.
Arajiga anatengeneza seti ya Waamuzi na waamuzi wenzake kutoka Tanzania Hamdan Ally ambaye atakuwa Mwamuzi Msaidizi namba moja, Ally Ramadhani Msaidizi namba mbili na Nasir Salum ambaye atakuwa mwamuzi wa akiba.
Katika mechi hiyo itakayochezwa Novemba 12, 2026, Kamishna wa mchezo atakuwa Wadjiri Godje kutoka Cameroon na Mtathimini wa Waamuzi ni Aboubacar Doumbouya kutoka Guinea.


