Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Leodger Tenga, amewataka wahitimu wa mafunzo ya juu ya Uongozi na Usimamizi wa Michezo (Advanced Sport Management Course) Awamu ya tatu, kutumia maarifa waliyoyapata kuimarisha usimamizi na maendeleo ya michezo nchini.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vyeti vya mafunzo hayo yanayotolewa na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Tenga amesema changamoto kubwa katika sekta ya michezo ni upungufu wa wataalamu wa usimamizi, hivyo elimu ya michezo inapaswa kupewa kipaumbele kwa viongozi na watendaji wa taasisi za michezo.
Amesisitiza kuwa maendeleo ya michezo yanahitaji uongozi wenye weledi, uadilifu, uwajibikaji na mtazamo wa kimkakati, huku akiwataka wahitimu kwenda kutumia elimu hiyo kwa vitendo na kuwa mfano katika Taasisi zao.
Washiriki 15 wamekabidhiwa vyeti leo kwenye hafla iliyofanyika Makao Makuu ya TFF, Karume, Ilala.


