Kocha Mkuu wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania Bara, ‘Kilimanjaro Stars’, Ammy Conrad Ninje, ametaja kikosi cha wachezaji 20 kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji mwaka huu wa 2017. Ninje – Kocha wa Daraja ‘A’ la Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA), ametaja kikosi hicho leo Jumamosi Novemba 18, 2017 kwenye Ukumbi 

Continue Reading

Ammy Conrad Ninje, ametangazwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwamba ndiye atakuwa Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ itakayoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji mwaka huu wa 2017. Katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Desemba 3, mwaka huu, Kilimanjaro Stars imepangwa Kundi ‘A’ pamoja wenyeji Kenya, Rwanda na Libya ambayo 

Continue Reading

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali limeandaa ligi ya soka la ufukweni kwa vyuo vya Mkoa wa Dar es Salaam mashindano yanayopangwa kuanza kesho Novemba 18, 2017. Ligi ya mwaka huu itafanyika katika Uwanja vya Escape One – Mikocheni uliopo Wilaya ya Kinondoni na itajumuisha jumla ya timu 16. 

Continue Reading

Tunaanza kwa kumshukuru Mungu kwa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, kusafiri salama kwenda na kurejea nchini alfajiri ya leo Jumanne Novemba 14, 2017. Pia TFF tunasema ahsante kwa namna ambavyo timu yetu imepambana na kutoka sare kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya wenyeji Benin 

Continue Reading

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), tayari limetangaza kuanza kwa mchakato kwa wanahabari kutapa vibali maalumu (accreditations) za kushuhudia na kuripoti habari za Fainali za Kombe za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Urusi, Juni, 2018. Kwa wanahabari wanaotaka vibali hivyo hawana budi kujisajili moja kwa moja TFF na wakapata uthibitisho kutoka Mkuu wa 

Continue Reading

Wakati Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, ikitarajiwa kuanza Novemba 26, 2017 katika vituo viwili vya Dar es Salaam na Arusha, tayari usajili wa msimu kwa timu zote 12, umekamilika. Kwa mujibu wa kalenda ya mashindano, usajili ulipangwa ufanyike kati ya Oktoba 25 na Novemba 12, mwaka huu na kwamba kuanzia leo Novemba 13 hadi 

Continue Reading

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison George Mwakyembe leo Jumamosi Novemba 11, amezindua Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 (AFCON U17) yakayofanyika Machi, 2019. “Kama unavyofahamu, Tanzania ilipokea heshima ya kuandaa mashindano ya AFCON 2019 kwa vijana chini 

Continue Reading

Matengenezo Uwanja Mkuu wa Taifa, Dar es Salaam, umekamilika na Mheshimiwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison George Mwakyembe, ameambiwa kuwa unaweza kuanza kutumika kuanzia Novemba 21, mwaka huu. Kwa msingi, Waziri Dk. Mwakyembe ametoa maagizo ya kuandaliwa mchezo maalumu wikiendi ya Novemba 24, 25 au 26 kupata mchezo mmoja wa ufunguzi 

Continue Reading

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), leo Novemba 10, 2017 wanakutana na viongozi wa vyuo kuzungumza taratibu zitakazotumika kwenye ligi ya soka la ufukweni itakayoanza Novemba 18, mpaka Desemba 9, mwaka huu kwenye Ufukwe wa Escape One, Mikocheni jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kitajadili usajili wa wachezaji, taratibu mbalimbali zitakazotumika pamoja na kupokea 

Continue Reading

Kikosi cha timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 23 Kilimanjaro Warriors kinaendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Karume chini ya walimu Kim Paulsen na Oscar Mirambo. Kikosi hicho cha wachezaji 35 kitafanyiwa mchujo na kubakia na wachezaji 25 watakaounda kikosi cha Olympic. Kambi hiyo iliyoanza Novemba 5,2017 itachukuwa siku 10 mpaka Novemba 16,2017.