Simba Queens yaanza vyema michuano ya CECAFA

    Timu ya Simba Queens ya Tanzania imeanza vyema michuano ya klabu bingwa Afrika ukanda wa CECAFA (CAF Women’s Champions League CECAFA Qualifiers 2026) baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Top Girl Academy ya Burundi.

    Mechi hiyo ya kwanza ya kundi C imechezwa Agosti 22, 2026 katika Uwanja wa Pele uliopo Kigali, Rwanda.

    Mabao yote ya Simba Queens yalifungwa kipindi cha pili. Bao la kwanza lilifungwa na Aisha Juma dakika ya 65 wakati Musakanda Kasamfula alifunga la pili dakika ya 80.

    Kwa ushindi huo Simba Queens inaongoza kundi C ikiwa na pointi tatu. Timu nyingine katika kundi hilo ni Top Girls Academy (Burundi) na Kenya Bullet Force FC.

    Simba Queens itacheza mechi ya pili dhidi ya Kenya Bullet Force FC Agosti 24 saa nane mchana katika Uwanja wa Pele.

    Timu kumi zinashiriki michuano hiyo ambazo ni Rayon Sport WFC (Rwanda), Yei Joint Stars FC (Sudani Kusini), Mafunzo FC (Zanzibar), Denden FC (Eritrea), CBE FC (Ethiopia), Kawempe Muslim Ladies (Uganda), FC Ujeco (Djibouti) Kenya Bullet Force FC (Kenya), Top Girls Academy FC (Burundi) na Simba Queens ya Tanzania.

    Share.