Timu ya Taifa ya Wanaume U20 (Ngorongoro Heroes) imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya kuwania kufuzu Fainali za AFCON Kanda ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), kwa kuichapa Ethiopia mabao 4-0 mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Ngorongoro Heroes yamefungwa na Bashiri Kibaila aliyefunga mabao mawili dakika ya 30 na 45, huku mawili mengine yakifungwa na Juma Sangwe dakika ya 53 na 55.

Ngorongoro Heroes wanatinga katika hiyo baada ya kuongoza Kundi A wakishinda michezo yake yote miwili. Mchezo wa kwanza waliichapa Rwanda mabao 3-0.


