Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) imeichabanga Botswana mabao 6-0 katika mechi ya kufuzu michuano ya Olimpiki 2028 itakayofanyika Los Angeles, nchini Marekani.

    Ukurasa wa mabao ya Twiga Stars ulifunguliwa na Aisha Mnunka dakika ya 38, kabla ya Hasnath Ubamba kufunga bao la pili dakika ya 43.

    Ester Maseke alifunga bao la tatu dakika ya 60, nahodha Oprah Clement aliifungia Twiga Stars bao la nne dakika ya 69, Mary Siame akapiga bao la tano dakika ya 74 na Enekia Lunyamila alifunga bao la sita na kukamilisha hesabu ya mabao.

    Twiga Stars imetinga raundi ya tatu kwa jumla ya mabao 7-0 baada ya kushinda katika mechi ya kwanza kwa bao 1-0 jijini Gaborone, Botswana.

    Kwa ushindi huo Twiga Stars itakutana na mshindi kati ya Ethiopia na Rwanda katika raundi ya tatu mechi zitakazochezwa kati ya Januari na Februari 2027.

    Share.