Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wavulana U17 (Serengeti Boys), imejiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya nusu fainali ya mashindano ya kufuzu AFCON 2027 Kanda ya CECAFA.

    Serengeti Boys imejiweka katika nafasi hiyo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Somalia katika mechi ya pili ya Kundi C.

    Kwa matokeo hayo Serengeti Boys wanaongoza Kundi C wakiwa na pointi 4 baada ya kushinda mechi ya kwanza dhidi ya Kenya kwa mabao 2-0.

    Serengeti Boys inasubiri matokeo ya mechi kati ya Kenya na Somalia ili kujua nafasi yao katika kundi hilo, lakini bado wana nafasi ya kusomba mbele kupitia timu iliyoshika nafasi ya pili kwa kuwa na matokeo mazuri.

    Hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo itachezwa Oktoba 17, 2026, wakati fainali itachezwa Oktoba 19 mwaka huu.

    Share.