Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) Simba Queens wameanza kampeni ya kutetea ubingwa wake kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kilimanjaro Wonders.

    Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa Ushirika, mjini Moshi, mabao ya Simba yalifungwa na Aisha Juma dakika ya 19, Senaf Demise dakika ya 28 kabla ya Asphalt Kasindo kujifunga dakika ya 56.

    Simba Queens ambao msimu uliopita walitwaa ubingwa huo kwa kutopoteza mechi hata moja baada ya kushinda 19 na sare tatu, wameanza kampeni yao ya kuhakikisha wanatetea taji lao msimu huu.

    Share.