Timu ya Yanga Princess imeibuka na ushindi mnene wa mabao 7-1 dhidi ya Kilimanjaro Wonders kwenye Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL).

    Mabao ya Yanga katika mechi hiyo iliyochezwa uwanja wa KMC yalifungwa na Salamata Kuoanda aliyefunga mabao manne katika dakika za 5, 16, 34 na 61.

    Nyota wengine wa Yanga waliokwamisha mpira wavuni ni Cynthia Masubgu dakika ya 21, Barakati Olaiya dakika ya 28 na Rehema Mohamed dakika ya 38 wakati bao la Kilimanjaro Wonders lilifungwa na Rahima Chile katika dakika ya 71.

    Mechi nyingine iliyochezwa leo, Alliance Girls iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Bunda Girls kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza.

    Share.