Timu ya Taifa ya Wavulana U17 (Serengeti Boys) imeanza kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Costa Rica katika Fainali za Kombe la Dunia 2026, Qatar.

    Katika mechi hiyo Serengeti Boys walitanguliwa kwa mabao 2-0 katika kipindi cha kwanza kabla ya kutoka nyuma katika kipindi cha pili na kusawazisha.

    Mabao ya Serengeti Boys yalifungwa na Faraji Kayanda katika dakika ya 50 na 73 na kuifanya kuondoka na pointi moja.

    Serengeti Boys iliyopo Kundi I, itashuka tena uwanjani Novemba 24, 2026 kuvaana na Brazil na mechi yake ya mwisho hatua ya makundi itakuwa dhidi ya Ireland itakayochezwa Novemba 27, 2026.

    Share.