Azam yatwaa ubingwa U2
Timu ya Azam imeilaza Yanga mabao 2-1 katika mechi ya fainali ya Ligi Kuu ya U20 ya NBC msimu wa 2025/2026.
Ushindi huo katika fainali hiyo iliyochezwa tarehe 1 Julai kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam umeifanya Azam kuibuka mabingwa.
Mabao ya Azam yalifungwa na Juma Mbwana dakika ya 11, na Adnan Rashid dakika ya 62 wakati lile la Yanga lilifungwa dakika ya 64 kupitia kwa Saleh Mahsen.
Katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu timu ya Mbeya City iliifunga JKT Tanzania kwa penalti 4-2. Dakika 90 za kawaida zilimalizika kwa timu hizo kufungana mabao 2-2.
Timu zilizofanikiwa kucheza Hatua ya Nane Bora kwenye Ligi hiyo ni Azam, Dodoma Jiji, JKT Tanzania, Mashujaa, Mbeya City, Mtibwa Sugar, Simba, na Yanga.


