Simba ni kishindo Kombe la CRDB
Simba imeingia kwa kishindo nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB baada ya kuikung’uta TRA United mabao 4-0.
Mechi hiyo ya robo fainali ya michuano hiyo ilifanyika tarehe 17 Mei katika Uwanja wa KMC jijini Dar es Salaam.
Katika hatua ya nusu fainali Simba itakabiliana na Coastal Union FC ambayo tarehe 16 Mei iliing’oa Singida Black Stars kwa mabao 4-2 kwenye mechi ya robo fainali iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Mechi zote za nusu fainali (Azam v Yanga), na Simba v Coastal Union) zitachezwa tarehe 20 Juni katika viwanja vitakavyotangazwa baadaye na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).


