Polisi Moro na Ruvu Shootings zashuka daraja.

Ligi Kuu ya Vodacom itashirikisha timu 16 kuanzia msimu wa 2015/2016. Kabla ya hapo ligi hii kubwa nchini inayodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano Vodacom Tanzania ilikuwa ikishirikisha timu 14. Timu za Polisi Morogoro na Ruvu Shootings zimeshuka daraja na timu za Majimaji kutoka Songea, African Sports kutoka Tanga, Toto Africans na Mwadui FC zimepanda daraja kushiriki Ligi Kuu ya Vodacom.